PARIS, Ufaransa
MATAJIRI wa klabu ya PSG wameingia kwenye harakati za kuinasa saini ya beki wa pembeni wa Atletico Madrid, Malo Gusto.
Kocha wa PSG, Luis Enrique, Gusto ni beki anayefaa kumpa changamoto mlinzi wake wa kulia raia wa Morocco, Achraf Hakimi.
Nyota mwingine wa Atletico aliyeingia kwenye rada za PSG ni kiungo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 25, Alex Baena.
Mbali na kiungo mshambulaji, Baena ni ‘kiraka’ anayetumika pia kucheza winga ya kushoto, straika na kiungo wa kati.
Msimu huu wa 2026-27 umekuwa mzuri kwa Baena mwenye umri wa miaka 25 kwani amefunga mabao manne na kutoa ‘asisti’ mbili katika mechi tisa msimu huu.


