LONDON, Uingereza
KOCHA wa zamani wa Bolton, Sam Allardyce, amepongeza kitendo cha staa wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, kuondoshwa kikosini.
Allardyce amemtaja kocha wa Ureno, Jorge Jesus, kuwa ni shujaa aliyethubutu kumshughulikia mchezaji huyo.
Ronaldo aliondoka kambini kabla ya Ureno kuivaa Denmark hivi karibuni baada ya Jesus alimwambia hatomtumia kwenye mechi hiyo.
“Kocha [Jesus] alifanya uamuzi mgumu kumwambia kwamba kwa umri wake haendani na mfumo anaotaka timu icheze,” amesema.
Tangu alipoondoka kikosini, Ureno imeendelea kufanya vizuri kwenye mechi zake, hiyo ikiibua sintofahamu juu ya hatima ya supastaa huyo.


