15.3 C
New York

Bruno: Ronaldo aheshimiwe, ni nembo ya Ureno

Published:

LISBON, Ureno

LICHA ya yote yaliyotokea, kiungo wa timu ya soka ya Taifa ya Ureno, Bruno Fernandes, anaamini bado Cristiano Ronaldo anapaswa kupewa heshima anayostahili.

Kauli ya Bruno imekuja wakati huu Ronaldo akikosolewa vikali kwa uamuzi wake wa kuondoka kambini kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya [Nations League] dhidi ya Denmark.

Ronaldo aliondoka baada ya kugundua kuwa hakuwa kwenye mipango ya kocha wa sasa, Jorge Jesus.

Licha ya kukosekana kwake, bado Ureno iliweza kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Denmark, hivyo mashabiki kumgeukia na kuanza kumponda huko mitandaoni.

Akizungumzia hilo, Bruno amesema: “… Kama nilivyowahi kusema, Cristiano ndiye na atabaki kuwa nembo kubwa zaidi ya timu yetu ya taifa.

“Cristiano Ronaldo anastahili heshima kutoka kwa watu wote wa Ureno, bila kujali wanaompenda na wanaomchukia.”

Related articles

Recent articles