18.3 C
New York

Lewandowski amegoma kuzeeka, atupia ‘hat-trick’

Published:

WARSAW, Poland

LICHA ya umri wake wa miaka 38, straika wa timu ya soka ya Taifa ya Poland, Robert Lewandowski, ameendeleza moto wake wa kucheka na nyavu baada ya kutupia ‘hat-trick’ katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Romania.

Romania ilimaliza dakika 90 za mchezo huo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya [Nations League] ikiwa pungufu baada ya beki wa Tottenham, Radu Dragusin, kulimwa kadi nyekundu dakika ya 22.

Lewandowski alianza kuziona nyavu za Poland kwa mkwaju wa penalti, kabla ya kuongeza mengine mawili katika kipindi cha pili cha mechi hiyo.

Aidha, Romania haikuwa na bahati katika mechi hiyo kwani licha ya kadi nyekundu, nyota wake wawili, Piotr Zielinski na Jan Bednarek, nao walijifunga.

Kwa sasa, Lewandowski amefikisha ‘hat-trick’ saba akiwa na timu ya taifa. Kwa ujumla, ameshaifungia Poland jumla ya mabao 92.

Related articles

Recent articles