MILAN, Italia
NYOTA wa AC Milan, Zachary Athekame, ameweka wazi kuwa ameachana na wazo lake la kuitumikia timu ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’.
Shirikisho la Soka la Nigeria [NFF] lilikuwa na matumaini makubwa ya kumshawishi mchezaji huyo mzaliwa wa Geneva, Uswis, kuiwakilisha ‘Super Eagles’.
Hata hivyo, beki wa kulia huyo anayekipiga Lyon kwa mkopo amechagua njia tofauti na sasa ataitumikia Uswis.
Baba yake mzazi ni raia wa Nigeria na Athekame alikuwa sehemu ya kikosi cha Uswis kilichopata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya North Macedonia.
Kocha wa Uswis, Murat Yakin, alishawishika kumwita kikosini baada ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 21 kuuanza vizuri msimu huu wa Ligue 1, akifunga mabao mawili na kutoa ‘asisti’ mbili katika mechi tano.


