LONDON, Uingereza
NI wiki 12 tu zimepita tangu timu ya soka ya Taifa ya Hispania ilipotwaa taji la fainali za Kombe la Dunia.
Kwa sasa, mechi za timu za taifa zimerejea, ambapo ni michuano ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya [UEFA Nations League] ndizo zinazochezwa.
Wakati huo huo, uhondo mwingine ni kwamba vigogo Ujerumani, Uholanzi na Ufaransa wako chini ya makocha wapya na wageni katika soka la kimataifa.
Jurgen Klopp (Ujerumani)
Alifanya makubwa kwa miaka tisa aliyokuwa Liverpool, ambapo ameiachia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na lile la Ligi Kuu. Julai, 2026, alipewa mikoba ya kuinoa Ujerumani.
Kabla ya kuajiriwa Klopp, Ujerumani ilikuwa chini ya Julian Nagelsmann ambaye alijiuzulu baada ya kufanya vibaya Kombe la Dunia mwaka 2026.
Xavi (Uholanzi)
Mhispania huyo amevunja rekodi na kuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuinoa Uholanzi baada ya miaka zaidi ya 50 kupita.
Kabla ya kuajiriwa, Xavi alikuwa nje ya kazi tangu alipoondoka Barcelona mwaka 2024. Amechukua nafasi ya kocha mzawa, Ronald Koeman, ambaye alijiuzulu baada ya Kombe la Dunia [2026].
Zinedine Zidane (Ufaransa)
Julai, 2026, Shirikisho la Soka la Ufaransa lilimtangaza kiungo wake wa zamani, Zidane, kuwa kocha mpya wa timu ya taifa akichukua mikoba ya Didier Deschamps aliyekuwa ameinoa kwa miaka 14.
Zidane [54], alikuwa mchezaji wakati Ufaransa inatwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 na ana tuzo ya Ballon d’Or. Mafanikio yake makubwa kwenye ukocha ni kuipa Real Madrid mataji mawili ya La Liga na matatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa.
Jorge Jesus [Ureno]
Ureno ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya [Nations League] na sasa nayo iko chini ya kocha mpya, Jorge Jesus. Anaingia kwa mara ya kwanza kwenye ukocha wa timu za taifa akiwa na umri wa miaka 72.
Kocha huyo wa zamani wa Al-Hilal ya Saudi Arabia ameajiriwa kuchukua nafasi ya raia wa Ubelgiji, Roberto Martinez. Je, atatoboa na kuipa mafanikio Ureno ya Cristiano Ronaldo?
Roberto Mancini [Italia]
Kocha mzawa huyo aliiongoza Italia kutwaa kutwaa taji la fainali za EURO 2020. Mancini amerejea kwenye benchi baada ya muda mfupi alioinoa Saudi Arabia.
Mancini anafahamika vizuri kwa mafanikio yake makubwa katika soka la Ulaya, hasa alipokuwa kwenye benchi la ufundi la Inter Milan na Manchester City.
Slaven Bilic [Croatia]
Aliondoka kwenye benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Croatia mwaka 2012 baada ya kuinoa kwa miaka sita. Bilic, mmoja ya makocha wakongwe Ulaya, amerejea kazini.
Je, baada ya miaka 14 ya kuwa pembeni, amerejea kuipa mafanikio timu yake ya Taifa ya Croatia? Kwa ufupi, ndiye kocha aliyempa nafasi Luka Modric na sasa ni miongoni mwa wachezaji wenye heshima kubwa nchini humo.


