MUNICH, Ujerumani
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Colombia, Luis Diaz, anaamini staa mwenzake katika kikosi cha Bayern Munich, Harry Kane, ndiye anayestahili tuzo ya Ballon d’Or ya mwaka huu.
Diaz, nyota wa zamani wa Liverpool, ameyasema hayo katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha ESPN.
“Kwa upande wangu, [Kane] ndiye chaguo la kwanza kushinda [Ballon d’Or]. Ni matumaini yangu, kwamba atafanikiwa katika hilo,” amesema Diaz.
Kane amekuwa akitajwa zaidi katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo, licha ya ushindani alionao mbele ya Kylian Mbappe wa Real Madrid na staa wa Barcelona, Lamine Yamal.
Kwa sasa, tayari imeshatangazwa orodha ya wachezaji 30 wanaoiwania tuzo hiyo, ingawa watatu hao ndiyo wanaozungumziwa zaidi.


