13.7 C
New York

Boateng aanza kazi ya ukocha

Published:

MANCHESTER, Uingereza

BEKI wa zamani wa Manchester City na timu ya Taifa ya Ujerumani, Jerome Boateng, ametangazwa kuwa kocha msaidizi wa Trabzonspor ya Ligi Kuu ya Uturuki.

Boateng aliyewahi pia kucheza Bayern Munich, alistaafu kucheza soka la kulipwa Septemba 19, 2026, akiwa na umri wa miaka 37.

Akiwa Bayern, aliweza kutwaa mataji kadhaa, yakiwamo tisa ya Ligi Kuu ya Ujerumani [Bundesliga], mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na matano ya DFB Cup.

Wakati huo huo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014.

Katika maisha yake ya soka, Boateng aliwahi kupita katika klabu za Hertha BSC, Hamburger SV, Olympique Lyon, US Salernitana na LASK.

Related articles

Recent articles