13.7 C
New York

Mbappe aizima Uturuki, Ubelgiji yaitandika Italia

Published:

PARIS, Ufaransa

MECHI kadha za Ligi ya Mataifa ya Ulaya [Nations League] zilichezwa jana Septemba 25, 2026, huku timu ya Taifa ya Ufaransa ikiitandika Uturuki bao 1-0, mfungaji akiwa ni nahodha wa kikosi, Kylian Mbappe.

Katika mechi hiyo, staa wa Uturuki, Ugurcan Cakır, alishindwa kumaliza baada ya kulimwa kadi nyekundu dakika ya 87.

Mchezo mwingine ni ule ulioishuhudia Ubelgiji ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Italia, wakati Ukraine iliifunga Hungary bao 1-0.

Kama ilivyotokea kwa Uturuki, Ukraine ilimaliza mchezo ikiwa na wachezaji pungufu baada ya Oleksandr Nazarenko kulimwa kadi nyekundu.

Matokeo ya mechi zingine za jana ni kama ifuatavyo; Sweden 2–1 Romania, Montenegro 2–1 Cyprus, Northern Ireland 1–0 Georgia, Armenia 2–0 Latvia, na Poland 0–0 Bosnia.

Related articles

Recent articles