NEW YORK, Marekani
WIZARA ya Mambo ya Nje ya Uingereza imeitahadharisha Iran ikiitaka kuacha jaribio lolote la kuishambulia nchi hiyo.
Aliyetuma ujumbe huo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ed Miliband, akisema hawatosita kujibu mapigo endapo Iran itaanzisha mashambulizi.
Ed Miliband amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.
Uingereza imelaani mashambulizi dhidi ya raia wao wa Kiyahudi wanaoishi Iran. Pia, wenza wawili raia wa Uingereza wanashikiliwa katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.
Iran imekuwa kwenye uadui mkubwa na mataifa yenye uhusiano na Marekani na Israel, ikiwamo Uingereza. Marekani na Israel yaliishambulia Iran kuanzia Februari 28, 2026, na vita hivyo vimeendelea hadi sasa.


