MADRID, Hispania
ZIMEIBUKA taarifa kuwa staa wa Real Madrid, Kylian Mbappe, anajaribu kununua kura za tuzo za mwaka huu za Ballon d’Or.
Hayo yamefichuliwa na kiungo wa zamani wa PSG, Jerome Rothen, akisema Mbappe mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akiendesha kampeni za kushawishi kupigiwa kura.
Kwa mujibu wa Rothen, Mbappe amekuwa akijinasibu hadharani kuwa ndiye anayestahili tuzo hiyo na kwa kauli hiyo ni wazi anajaribu kuvuna ushawishi.
Katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha RMC Sport, Rothen amesema: “Nitakuwa makini na kile ninachokieleza kwa kuwa najua kitazua mitazamo tofauti lakini haitonizuia kusema.”
Mshindi wa tuzo hiyo anatarajiwa kutangazwa Oktoba 26, 2026, huku Mbappe akikabiliwa na ushindani mkali mbele ya Lamine Yamal, Harry Kane, Lionel Messi na Ousmane Dembele.


