ALGIERS, Algeria
KIUNGO wa zamani wa Rangers ya Ligi Kuu ya Scotland, Brahim Hemdani, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya soka ya Taifa ya Algeria na mtihani alionao ni kuiwezesha kufuzu AFCON 2027.
Hemdani anachukua nafasi ya Vladimir Petkovic, ambaye alifungashiwa virago baada ya Algeria kufanya vibaya katika fainali zilizopita za Kombe la Dunia.
Algeria iliishia hatua ya 32 baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Uswis. Ilikuwa ni mara ya pili kwa timu hiyo kuvuka makundi.
Aidha, Algeria iliishia robo fainali ya AFCON wakati michuano hiyo ilipofanyika nchini Nigeria mwanzoni mwa mwaka huu (2026).
Katika maisha yake ya uchezaji wa soka, Hemdani aliyezaliwa Ufaransa alicheza mechi mbili tu akiwa na timu ya Taifa ya Algeria.
Alijiunga na Rangers mwaka 2005, ambapo alicheza mechi 108, kabla ya kuondoka klabuni hapo mwaka 2009 na hivi karibuni alikuwa na U-21 ya Algeria.


