MADRID, Hispania
KOCHA wa Atletico Madrid, Diego Simeone, amesema wapinzani wao, Athletic Bilbao, walikuwa wazuri kwenye ulinzi na ndiyo maana ikawa ngumu kwa vijana wake kupata ushindi.
Katika mechi hiyo ya La Liga iliyochezwa jana Septemba 5, 2026, Atletico walidondosha pointi zote tatu kwa kichapo cha mabao 3-0.
Bilbao walipata ushindi huo wa nyumbani kupitia mabao ya Nico Williams, Robert Navarro na Oihan Sancet.
“Ukweli ni kwamba tuliianza mechi vizuri kama tulivyotarajia. Lakini zile dakika tano (za mwanzo wa kipindi cha pili) zilituma ujumbe. Tunapaswa kuamka na kufanyia kazi mapungufu,” amesema.
Baada ya maumivu hayo, Atletico sasa wanajiandaa kukabiliana na Liverpool katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa Jumatano ya wiki ijayo.


