22.3 C
New York

EU yapiga marufuku nyama kutoka Brazil

Published:

RIO, Brazil

UMOJA wa Ulaya (EU) umeweka katazo kwa nchi zake kuingiza nyama kutoka Brazil, ikieleza kuwa hatua hiyo inatokana na sababu za kiafya.

Kwa mujibu wa Tume ya Ulaya, Brazil imeshindwa kutoa uhakika wa viwango vya usafirishaji wa nyama.

Mei, 2026, EU iliiweka Brazil katika orodha ya nchi zisizofuata taratibu za matumizi ya dawa za kuzuia bakteria kwa wanyama.

“Brazil haitoruhusiwa kusafirisha barani Ulaya vyakula vitokanavyo na wanyama kwa matumizi ya binadamu,” imeeleza taarifa ya EU.

Ni kwa maana hiyo, katazo hilo litaathiri sekta za ufugaji, nyama, mayai na asali na EU haijaweka wazi ukomo wa katazo lao kwa Brazil.

Related articles

Recent articles