24 C
New York

Kigogo wa jeshi Marekani ajiuzulu

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

KATIBU wa jeshi la Marekani, Dan Driscoll, amewasilisha barua ya kujiuzulu nafasi hiyo ikiwa ni miezi 18 tu imepita tangu alipoteuliwa.

Taarifa za kung’atuka kwake zimethibitishwa na Shirika la Habari la CBS, washirika wakubwa wa BBC.

Kwa mujibu wa CBS, Driscoll amefikia uamuzi wa kujiweka kando baada ya ugomvi wake na Katibu wa Wizara ya Ulinzi, Pete Hegseth.

Driscoll (41), ndiye Katibu wa jeshi mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Marekani na wakati fulani Rais Donald Trump alimfananisha na ndege isiyo na rubani kutokana na uchapakazi wake.

Kwa muda mfupi alioshika nafasi hiyo, Driscoll alisifika kwa kusimamia kwa ufanisi operesheni za kijeshi, pia akiwa sehemu muhimu ya kampeni ya ‘Make America Strong Again’.

Wakati huo huo, Driscoll anakuwa kiongozi mwingine wa ngazi za juu katika jeshi la Marekani kutangaza kujiuzulu.

Miongoni mwao ni aliyekuwa kiongozi wa jeshi la majini, John Phelan, ambaye aliachia ngazi Aprili, 2026.

Related articles

Recent articles