Na mwandishi wetu, Gazetini
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Asharose Migiro, amesema Halmashauri Kuu ya CCM imeamua kumfukuza uanachama aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi, baada ya kubaini ukiukwaji wa Katiba na kanuni za chama.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Jumatano, Agosti 26, 2026, Dk. Migiro amesema suala hilo lilijadiliwa kwa kina katika kikao hicho, huku agenda ya nidhamu na maadili ikiwa miongoni mwa mambo yaliyowasilishwa.
“Baada ya kuzingatia taarifa zote zilizotolewa, ilibitika kwamba Katiba ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na kanuni zake zilikiukwa. Kufuatia hayo, kwa pamoja, Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ilipitisha uamuzi kwamba kutokana na mienendo iliyokiuka kanuni zetu zinazohusu nidhamu na maadili, Dk. Emmanuel Nchimbi afukuzwe uanachama kwa mujibu wa kanuni zetu,” amesema Dk. Migiro.


