19.1 C
New York

Salah kazi imeanza, atupia mawili Uturuki

Published:

ISTANBUL, Uturuki

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Liverpool, Mohamed Salah, amefunga mabao mawili katika mechi yake ya kwanza aliyoingia ‘first eleven’ akiwa na timu yake mpya ya Trabzonspor ya Uturuki.

Salah alipachika mabao hayo akiiwezesha Trabzonspor kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Istanbul Basaksehir. Mchezo huo ni wa Ligi Kuu ya Super Lig.

Mechi hiyo ilikuwa ya tatu kwa Salah akiwa na Trabzonspor lakini ya kwanza akiwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Itakumbukwa, alitokea benchi katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Kasimpasa na ile ya ‘playoff’ ya Ligi ya Europa dhidi ya Ferencvaros.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34,alijiunga na Trabzonspor majira haya ya kiangazi baada ya kuachana na Liverpool.

Related articles

Recent articles