NYON, Uswis
RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ametakiwa kutokuhudhuria michuano ya soka ya U-14 inayofanyika nchini Jamhuri ya Dominica.
Ushauri huo umetoka kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Amerika (CONCACAF), Victor Montagliani, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa FIFA.
Infantino amealikwa kama mgeni rasmi lakini Montagliani anaamini taswira ya FIFA imeharibika, hivyo Infantino hastahili heshima hiyo.
“Vyombo vya habari vitajikita kwake, hivyo kuathiri umuhimu wa kiufundi wa mashindano hayo,” ameandika Montagliani huko mitandaoni.
Kwa muda sasa, Infantino amekuwa kwenye presha, akikosolewa kwa hatua yake iliyofeli ya kuuza hisa za mashindano yote ya FIFA, ikiwamo Kombe la Dunia.


