24.7 C
New York

Messi atozwa faini kwa kumpiga mtu kofi

Published:

MIAMI, Marekani

SUPASTAA wa Inter Miami, Lionel Messi, ametozwa faini kwa kosa la kumpiga kofi nyota wa Philadelphia Union, Quinn Sullivan.

Mbali na Messi, Ian Fray wa Inter Miami naye ametozwa faini kwa kumkaba koo mchezaji mwingine wa Philadelphia katika mchezo huo wa sare ya mabao 2-2.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS) iliyochezwa Jumatano ya wiki hii, Messi raia wa Argentina alifunga bao moja na kutoa asisti.

Hata hivyo, kama itakumbukwa, dakika 90 za mechi hiyo zilimalizika zikiwa zimeshuhudia kadi nyekundu mbili.

Aidha, waliolimwa kadi hizo ni staa wa Inter Miami, Yannick Bright, pamoja na kaka yake Sullivan aitwaye Cavan.

Related articles

Recent articles