24.9 C
New York

Mkwe wa Jux azua mjadala mitandaoni

Published:

LAGOS, Nigeria

ANAITWA Iyabo Ojo. Ni mwigizaji maarufu nchini Nigeria na mama mzazi wa bibiye Priscilla, ambaye ni mke wa staa wa Bongo Fleva, Juma Jux.

Sasa, bi. Iyabo mwenye umri wa miaka 48, amezua mjadala kwa mashabiki wake huko mitandaoni baada ya kusema mwanamke aliye ‘singo’ anafurahia maisha kuliko aliyeolewa.

Kwa mujibu wake, mwanamke aliye singo anainjoi anapata huduma ya ngono kwa kiwango kikubwa, ikilinganishwa na wanawake wengi walio kwenye ndoa.

Mama huyo wa watoto wawili, ameenda mbali zaidi na kusema ngono ina umuhimu mkubwa kwa afya ya mwanamke.

“Ngono ina maana kubwa sana katika afya ya mwanamke. Sababu ya wanawake wengi walio singo kuishi maisha ya furaha ni kwa sababu wanapata ngono vya kutosha,” amesema mwigizaji huyo.

Related articles

Recent articles