LONDON, Uingereza
KLABU ya Real Madrid haijaachana na mpango wake wa kumsajili kiungo wa Arsenal na timu ya soka ya Taifa ya Hispania, Martin Zubimendi.
Licha ya kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, kutaka mchezaji huyo asiuzwe, bado Madrid wanakomaa naye wakishinikiza kulipa dau la Pauni milioni 65.
Zubimendi atamaliza mkataba na Arsenal ifikapo Juni, 2030. Arsenal waliikataa ofa ya Liverpool mwaka jana.
Washika Bunduki walitumia Pauni milioni 51 kuinasa saini yake mwaka 2025, wakati huo akitokea Real Sociedad.
Kwa upande wake, Zubimendi haoneshi kuvutiwa na mpango wowote wa kuondoka Emirates majira haya ya kiangazi.


