MUNICH, Ujerumani
KLABU mbili za Barcelona na Tottenham zimeingia kwenye vita ya kuiwania saini ya mpachikaji mabao hatari wa Bayern Munich, Harry Kane.
Kane (33), anatarajiwa kurejea Ujerumani wiki hii baada ya mapumziko ya fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika Julai 19, 2026.
Kwa sasa, amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na ameonesha nia ya kuongeza miaka mitatu ya kubaki Allianz Arena.
Barcelona wameendelea kuishinikiza Bayern imwachie, ikiamini Muingereza huyo atafaa kuziba pengo la Robert Lewandowski aliyeondoka.
Wakati huo huo, Barca wamekuwa wakihusishwa na mpachikaji mabao wa kimataifa wa Argentina anayekipiga Atletico Madrid, Julian Alvarez.


