PARIS, Ufaransa
MTANDAO wa takwimu wa Polymarket SuperComputer umeipa PSG nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao wa 2026-27.
Kwa mujibu wa Supercomputer, matajiri hao wa Jiji la Paris wana uwezekano wa asilimia 14, sawa na Real Madrid na Bayern Munich.
Manchester City, mabingwa mara moja wa mashindano hayo, wao wamepewa asilimia 13 ya kubeba tena msimu ujao.
Hata hivyo, ubashiri huo wa Supercomputer unakuja wakati ambao bado Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) halijachezesha droo yake.
Ratiba ya UEFA kwa msimu wa 2026-27 inaonesha kuwa droo ya Ligi ya Mabingwa itachezeshwa Agosti 27, 2026.


