MANCHESTER, Uingereza
MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Antoine Semenyo, amesifia aina ya uchezaji wa timu hiyo chini ya kocha mpya raia wa Italia, Enzo Maresca.
Semenyo ametoa kauli hiyo baada ya Man City kufungwa na Inter Milan kwa penalty 3-1 katika mchezo wa kwanza chini ya Maresca.
Katika mchezo huo wa kirafiki uliochezwa Hong Kong, Man City walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 14 kupitia kwa Divin Mubama lakini Benjamin Pavard aliisawazishia Inter dakika sita tu baadaye.
Licha ya kupoteza, Semenyo ameeleza kukoshwa na kiwango kizuri kilichooneshwa na Man City, hasa katika dakika 45 za kwanza.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ghana alionesha kiwango kizuri, ambapo kasi yake ilimpa wakati mgumu beki wa pembeni wa Inter, Andy Diouf.


