24.4 C
New York

Kocha atimka Man United kisa ‘ubahili’ sokoni

Published:

MANCHESTER, Uingereza

PIGO zito! Kocha wa timu ya soka ya wanawake ya klabu ya Manchester United, Marc Skinner, amejiuzulu, zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya uanza kwa msimu mpya wa 2026-27.

Skinner mwenye umri wa miaka 43, amekuwa kwenye benchi la ufundi la Man United kwa miaka mitano na aliipa taji la FA mwaka 2024.

Pia, kocha huyo ndiye aliyeiwezesha timu hiyo kufika kwa mara ya kwanza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2025.

Kwa mujibu wa taarifa, kilichomng’oa kwenye benchi ni kuona mabosi hawako ‘siriazi’ katika dirisha la usajili majira haya ya kiangazi.

Wakat huo huo, mashabiki wa Man United pia wameeleza kutokuvutiwa na namna uongozi wa klabu hiyo ulivyo na kasi ndogo ya usajili, ikilinganishwa na wapinzani wao Manchester City, Arsenal na Chelsea.

Related articles

Recent articles