LIMA, Peru
MAHAKAMA ya Katiba ya Peru imeamuru kuachiwa huru kwa Rais wa zamani wa Taifa hilo, Ollanta Humala, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani.
Humala (64), alikumbana na hukumu hiyo katika kesi yake ya rushwa, ikielezwa kuwa alijinufaisha na mkataba alioingia na kampuni ya ujenzi ya Brazil inayoitwa Odebrecht.
Pia, kiongozi na mkewe, Nadine Heredia, walishutumiwa kwa utakashikaji fedha kwa kushirikiana na Serikali ya nchi jirani ya Venezuela.
Kabla ya hukumu hiyo kutenguliwa, Humala alikuwa kwenye gereza lililoko Mashariki mwa Mji Mkuu wa Lima, ambako viongozi wengi wa Serikali wanatumikia vifungo vyao.
Ifahamike kuwa Humala aliyewahi kuwa ofisa wa jeshi, alikuwa Rais wa Peru kwa miaka mitano, kuanzia mwaka 2011 hadi 2016.


