22.9 C
New York

Vita ya makocha wapya EPL 2026-27

Published:

LONDON, Uingereza

MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya England (EPL) utaanza Agosti 21, 2026, ukitarajiwa kumalizika Mei 30, 2027. Ni msimu wa 35 tangu michuano hiyo ilipoanzishwa.

Safari hii, Washika Bunduki wa London, Arsenal, wanaingia kama mabingwa watetetezi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.

Pia, klabu tatu mpya – Coventry City, Hull City na Ipswich Town – zimeingia kuchukua nafasi ya Burnley, West Ham na Wolves zilizoshuka daraja msimu uliopita (2025-26).

Wakati huo huo, makocha Pep Guardiola na Arne Slot hawatokuwepo katika mabenchi ya ufundi ya Manchester City na Liverpool.

Na badala yake, nafasi zao zimechukuliwa na Enzo Maresca aliyetua Man City na Andoni Iraola aliyejiunga na Liverpool akitokea Bournemouth.

Kwa upande wa Chelsea, wao wana kocha mpya, Xabi Alonso, ambaye alifukuzwa Real Madrid akiwa ameiongoza katika mechi 34.

Chelsea ilikuwa chini ya makocha watatu tofauti katika msimu uliopita, huku kocha aliyetoka Madrid, Alvaro Arbeloa, akitua EPL kuliongoza benchi la ufundi la Fulham.

Makocha wengine wapya EPL kwa msimu wa 2026-27 ni Marco Rose (Bournemouth), Pierre Sage (Crystal Palace), Gary O’Neil (Ipswich Town) na Oliver Glasner (Nottingham Forest).

Related articles

Recent articles