26 C
New York

Shatta Wale afunguka ugomvi wake na Burna Boy

Published:

ACCRA, Ghana

STAAA wa muziki nchini Ghana, Shatta Wale, ameeleza kilichosababisha uhusiano wake mbaya na mkali wa Afrobeats, Burna Boy.

Wawili hao waliwahi kuwa washikaji wakubwa, ikiwamo Burna Boy kwenda Ghana na kufikia kwa Shatta Wale.

Sasa, kwa mujibu wa Shatta Wale, chanzo cha kuwa ‘chui na paka’ ni Burna Boy kuhisi ametoka na mpenzi wake.

Katika mahojiano yake, Shatta Wale amesema hisia hizo zilikuja wakati Burna Boy alipomtembelea nchini Ghana miaka kadhaa iliyopita.

“Nilimkaribisha vizuri Burna Boy, nikampa kila kitu, yakiwamo magari, ili ajisikie yuko nyumbani,” amesema Shatta Wale.

Akieleza zaidi, amesema watu wa karibu wa Burna Boy ndiyo walioanza kusambaza taarifa hizo za uongo, kwamba amemchukulia mpenzi wake.

Aidha, Shatta Wale amesema hana tatizo na Burna Boy, licha ya mwenzake huyo kuendelea kutokupokea simu wala kujibu meseji zake hadi leo hii.

Related articles

Recent articles