29 C
New York

Waisrael washutumiwa kuchoma misikiti ya Wapalestina

Published:

JERUSALEM, Palestina

RAIA wa Israel wanaoishi West Bank wameripotiwa kuchomo moto misikiti, magari na mashamba ya Wapalestina katika eneo hilo.

Madai hayo yanakuja zikiwa ni siku mbili tangu yalipozuka mapigano makali kati ya raia hao wa Israel na wenzao wa Palestina jirani na Kijiji cha Tal.

Katika mapigano hayo, raia wa Palestina wanne walifariki, huku wawili wa Israel nao wakiripotiwa kupoteza maisha.

Akizungumzia tukio hilo, Meya wa Qusra, Abdul Azim Wadi, amesema raia wa Israel wamechora kwenye kuta za misikiti jumbe za vitisho dhidi ya wenzao hao wa Palestina.

Kwa upande wake, jeshi la Israel limekiri kuzipokea taarifa hizo, likiahidi kutuma kikosi katika maeneo hayo kwa ajili ya uchunguzi wa kile kilichotokea.

Related articles

Recent articles