29 C
New York

Jurgen Klopp: ‘Nabii’ aliyekabidhiwa mzigo mzito Ujerumani

Published:

MUNICH, Ujerumani

WIKI chache zilizopita, alikuwa kwenye meza ya uchambuzi wa mechi za Kombe la Dunia akiishuhudia timu yake ya Taifa ya Ujerumani ikiondoshwa na Paraguay katika hatua ya 32 Bora.

Safari hii, Jurgen Klopp amepewa jukumu la kuliongoza benchi la ufundi, akichukua nafasi ya Julian Nagelsmann aliyetimuliwa baada ya matokeo hayo.

Kocha huyo wa zamani wa Liverpool amesaini mkataba wa miaka minne na ameongozana na wasaidizi wake aliifanya nao kazi klabuni hapo, Pep Lijnders na Peter Krawietz.

Akiwa Liverpool, alitwaa mataji makubwa mawili, Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu. Pia, aliipa Borussia Dortmund vikombe viwili vya Bundesliga (Ligi Kuu ya Ujerumani).

Sasa, anapaswa kuthibitisha ubora wake kwa kuiwezesha Ujerumani kufuzu fainali zijazo za Mataifa ya Ulaya (EURO 2028), pamoja na zile za Kombe la Dunia miaka miwili baadaye.

Mbaya zaidi kwake, ni imani kubwa waliyonayo baadhi ya mashabiki wa timu ya Taifa ya Ujerumani kwake, hasa kwa kile alichokifanya katika soka la ngazi ya klabu.

Ni mtazamo unaoungwa mkono pia na mkongwe wa soka la Ujerumani, Stefan Effenberg, na Mtendaji Mkuu wa Dortmund, Carsten Cramer, kwamba Klopp ni mtu sahihi kwao.

Hata hivyo, si wote wanaomkubali Klopp nchini Ujerumani na Mtihani ulio mbele yake ni kutokuwa na hiyo inatokana na kocha huyo kukosa uzoefu wa kufanya kazi na timu ya taifa.

Mkongwe wa Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ujerumani, Bastian Schweinsteiger, anaamini Ujerumani imekwama, hivyo ilihitaji kocha mwenye uzoefu wa kuzinoa timu za taifa.

Kwa maoni yake, Klopp hatoshi kumaliza tatizo la Ujerumani, ambayo ukiacha suala la ubingwa, haijafika hatua ya 16 Bora kwa misimu mitatu mfululizo ya Kombe la Dunia (2018, 2022 na 2026).

“Ni kweli ni namba moja (kwa mafanikio ya klabu) lakini unajiuliza; hakukuwa na chaguo jingine?,” amehoji
Schweinsteiger aliyekuwa kikosini wakati Ujerumani inatwaa Kombe la Dunia mwaka 2014.

Mechi ya kwanza ya Ujerumani ikiwa chini ya Klopp ni ya Septemba, 2026, dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Uholanzi. Ni mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya (UEFA Nations League).

Related articles

Recent articles