LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI mpya wa Arsenal, Christos Tzolis, amekabidhiwa jezi namba 17 kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya England (EPL) na michuano mingine.
Arsenal imetangaza usajili wa mchezaji huyo baada ya kukamilisha dili la kumng’oa katika kikosi cha Club Brugge ya Ubelgiji.
Tzolis mwenye umri wa miaka 24, ameondoka Club Brugge akiwa amecheza mechi 108, akifunga mabao 43 na kutoa ‘asisti’ 45.
Nyota huyo ameshaanza mazoezi na wenzake katika Uwanja wa mazoezi wa Arsenal wa Sobha Realty kwa ajili ya ‘pre-season’.
Akizungumzia dili hilo, Mkurugenzi wa Michezo wa Arsenal, Andrea Berta, amesema: “Ni furaha kwetu kukamilisha usajili wa Christos Tzolis.”


