MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester City inakazania mpango wa kumsajili mshambuliaji anayetaka kuondoka PSG, Ibrahim Mbaye.
Kwa sasa, taarifa zinaeleza kuwa Man City imeanza mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo, Jorge Mendes.
Baada ya kiwango kizuri msimu uliopita, Msenegal huyo mwenye umri wa miaka 18 ana thamani ya Pauni milioni 51 na mkataba wake na PSG utakwisha mwaka 2028.
Kwa upande wao, Man City wanaamini Mbappe anafaa kuziba pengo la Savinho anayekaribia kujiunga na vigogo wa London, Tottenham.
Hata hivyo, matajiri wa Etihad hawatomwachia Mbrazil huyo hadi pale watakapokuwa na uhakika wa kuinasa saini ya Mbaye.


