PARIS, Ufaransa
MATAJIRI wa klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia wanapambana kuinasa saini ya mshambuliaji wa PSG raia wa Ufaransa, Ousmane Dembele.
Al-Hilal wameibuka wakati huu uongozi wa PSG ukiendelea kumshawishi Dembele kusaini mkataba wa kumbakiza klabuni hapo.
Kwa sasa, mabosi wa PSG wako mezani na wachezaji wengi inaotaka kuwapa mikataba mipya, wakiwamo Dembele, Lucas Digne, Maghnes Akliouche, Yan Diomande na Bradley Barcola.
Dembele na Barcola wanahusishwa zaidi na mpango wa kuondoka klabuni hapo kipindi hiki cha usajili wa majira haya ya kiangazi.
Wakati huu, Barcola anahusishwa na vigogo wa mjini Merseyside, Liverpool, huku Arsenal nayo ikiripotiwa kuitaka saini yake.


