MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester United haijaacha kuipigania saini ya beki wa kati wa timu ya soka ya Taifa ya Colombia, Jhon Lucumi.
Nyota huyo wa Bologna aliwika kwenye fainali zilizopita za Kombe la Dunia na Juventus ndiyo ya kwanza kuhusishwa na saini yake.
Katika mkataba wake na klabu hiyo ya Italia, kuna kipengele kinachomruhusu kujiunga na klabu yoyote itakayoweka mezani kitita cha Pauni milioni 24.
Kwa mujibu wa ripoti, kocha wa Man United, Michael Carrick, ndiye anayelazimisha usajili wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28.
Wakati huo huo, klabu za Bayern Munich na Atletico Madrid nazo zimetajwa kumtolea macho staa huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 2.


