28.7 C
New York

Hii kiboko! Marais hawaendi uwanjani Argentina ikicheza

Published:

BUENOS AIRES, Argentina

HIVI unafahamu kuwa marais wa Argentina wamekuwa makini kuhudhuria viwanjani na wengine hubaki nyumbani pindi timu yao ya soka ya Taifa inapocheza mechi muhimu?

Ndiyo, kwa utamaduni wa muda mrefu nchini humo, rais anaweza kuipa ‘gundu’ timu ya taifa endapo atakuwa jukwaani.

Hii ilianzia wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1990, ambapo Rais wa wakati huo, Carlos Menem, alitembelea kambi ya timu ya taifa kuelekea mechi yao ya kwanza. Wakafungwa na Cameroon.

Baada ya mechi hiyo, mashabiki wa Argentina walimpachika jina la ‘mufa’, yaani ‘nuksi’. Tangu hapo hadi leo, hakuna rais aliyekwenda uwanjani kuitazama Argentina ikicheza.

Ndicho kilichotokea hata wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zilizomalizika hivi karibuni huko Marekani.

Rais Javier Milei hakuwa uwanjani wakati Argentina inacheza mechi ya kwanza, hadi ilipocheza fainali (dhidi ya Hispania).

Milei alitazama mechi zote nane, ikiwamo ya fainali ya Julai 19, 2026, akiwa sebuleni kwake nchini Argentina.

Kama sehemu ya imani yake, alivaa jaketi lilelile alilovaa katika mechi zote, akiamini lina mchango katika kuisaidia Argentina kushinda.

“Siku tuliyocheza na Uswis, nilijisikia joto sana. Nilipovua, (Uswis) wakapata bao. Nikalivaa, na tangu hapo sijavua tena,” alisema.

Related articles

Recent articles