30.9 C
New York

Dembele atabiriwa kuibeba Ballon d’Or

Published:

MUNICH, Ujerumani

MKONGWE wa soka la Ujerumani, Lothar Matthaus, amemtabiria staa wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, Ousmane Dembele, kutwaa tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.

Matthäus amesema Dembele ana nafasi kubwa kwa kuwa alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita akiwa na PSG, pia Ufaransa ilifika nusu fainali ya Kombe la Dunia hivi karibuni.

Katika orodha yake, lejendari huyo amewataka pia Kylian Mbappe na nahodha wa Hispania, Rodri, lakini amesema Dembele anastahili zaidi.

“Nafikiri Dembele ana nafasi zaidi, alishinda Ligi ya Mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo akiwa na PSG.

“Mbappe alikuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia lakini hakutwaa taji lolote akiwa na Real Madrid. Nitashangaa akipewa Ballon d’Or,” amesema.

Related articles

Recent articles