23.1 C
New York

Isabel wa Haaland naye siyo kinyonge

Published:

LONDON, Uingereza

NJE ya soka, Erling Haaland ni baba wa mtoto mmoja wa kiume aliyezaliwa Desemba, 2024. Pia, mwanasoka huyo ni mpenzi wa mrembo Isabel Haugseng Johansen.

Walijuana miaka mingi iliyopita, walipokutana wakiwa wachezaji wa timu za vijana katika klabu ya Bryne FK ya nchini Norway.

Isabel alikuwa timu ya wasichana klabuni hapo na alianza kuitumikia tangu akiwa na umri wa miaka 13.

Baadaye, Isabel na Haaland walipoteana baada ya bibiye huyo kuondoka Norway na kujiunga na Borussia Dortmund ya Ujerumani. Alitimka Bryne FK akiwa na mabao 23 katika mechi 36.

Haaland naye aliposajiliwa na Dortmund, akakutana na Isabel aliyekuwa timu ya wanawake ya klabu hiyo na uhusiano wao wa kimapenzi ukaanzia hapo.

Kwa sasa, Isabel hachezi tena soka na badala yake amekuwa akimsapoti Haaland kwa kwenda viwanjani katika mechi za Man City na timu ya Taifa ya Norway.

Wakati fulani, Isabel alizungumzia maisha yake ya soka, akikiri kuwa hakuwa mchezaji wa kiwango kikubwa uwanjani.

“Kwa kweli, sikuwa mzuri kwenye kukokota na kiufundi. Nilikuwa na kasi tu, nilikosa mabao sana,” amesema.

Baada ya kuachana na soka, Isabel ameingia mazima kwenye tasnia ya mitindo. Juni, 2026, aliingia kwa mara ya kwanza kwenye jarida maarufu la Norway, KK.

Kipindi hicho pia, kampuni ya vito ya Langgaard ya nchini Norway ilimpa ubalozi wa bidhaa zake.

Related articles

Recent articles