34.9 C
New York

Ramos: Shujaa anayefunikwa na kivuli cha Ronaldo

Published:

MIAMI, Marekani

AKITOKEA benchi, aliukuta mchezo ukiwa sare ya bao 1-1, kisha akafunga na kuiwezesha timu ya soka ya Taifa ya Ureno kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Croatia, matokeo yaliyowapeleka hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia.

Huyo si Cristiano Ronaldo wala Bruno Fernandes, bali ni Goncalo Ramos, akifanya hivyo katika mchezo wa hatua ya 32 Bora uliochezwa hivi karibuni mjini Toronto, Canada.

Ni straika ambaye aliwahi kufanya makubwa akiwa Benfica, kisha maisha yakawa magumu kwake alipotua PSG, kabla ya AC Milan kumnasa siku mbili kabla ya mechi dhidi ya Croatia.

Hata katika kikosi cha timu ya taifa, pia Ramos hakuweza kupata nafasi ya kuanza mbele ya Ronaldo.

Safari hii, Ramos aliyeingia uwanjani kuchukua nafasi ya nahodha wake huyo, ndiye aliyeibuka shujaa kwa bao lake lililoivusha timu kwenye wakati mgumu mbele ya Croatia ya Luka Modric.

Hiyo ilikuwa mechi yake ya pili msimu huu wa Kombe la Dunia, zote akitokea benchi kutokana na uwepo wa Ronaldo katika eneo la mshambuliaji wa kati.

Kama itakumbukwa, mchezo wake wa kwanza ni ule alitbaada yuingia ‘dakika za jioni’ walipokutana na DRC.

Kwa ujumla, nyota huyo amefikisha mabao manne na ‘asisti’ moja katika mechi sita za Kombe la Dunia alizowahi kucheza.

Related articles

Recent articles