34.9 C
New York

Simba yabeba FA, yamaliza ukame wa miaka minne

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

TUMERUDI! Simba imemaliza ukame wa miaka minne ya kupishana na taji la FA baada ya kulibeba msimu huu wa 2025-26 kwa kuifunga Azam bao 1-0.

Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa leo Julai 4, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Zanzibar, Simba ilipata bao pekee kwa Azam kujifunga kwa mpira wa faulo uliopigwa na nyota raia wa DRC, Elie Mpanzu.

Azam walilazimika kucheza sehemu kubwa ya mchezo ikiwa pungufu baada ya kiungo wake, Feisal Salum, kulimwa kadi nyekundu.

Mara ya mwisho kwa ubingwa wa michuano hiyo kutua Msimbazi ni msimu wa 2020-21, kisha Yanga ikanyakua mara nne mfululizo (2021-22, 2022-23, 2023-24 na 2024-25).

Kwa upande wao, Azam wameendelea kulisubiri taji la mashindano hayo tangu walipobeba msimu wa 2018-19.

Wekundu wa Msimbazi walitinga fainali kwa kuifunga Coastal Union mabao 4-0, wakati Azam wao waliwapata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga.

Related articles

Recent articles