MADRID, Hispania
WATU zaidi ya 1,000 wamepoteza maisha kutokana na magonjwa yanayohusiana na kuongezeka kwa joto nchini Hispania.
Taarifa hiyo inakuja wakati Hispania ikiwa imepata ongezeko kubwa zaidi la joto kuwahi kutokea kwa miaka ya hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Taasisi ya Afya ya Carlos III ya Hispania, mwezi Mei, 2026, watu 1,028 walipoteza maisha kwa changamoto za kiafya zinazosababishwa na joto kali.
Idadi hiyo ni kubwa mara mbili, ikilinganishwa na takwimu za vifo vya watu 407 vilivyoripotiwa Juni, 2025.
Juni 23, 2026, watu milioni 35.7, sawa na asilimia 73 ya raia wote wa Hispania, waliripotiwa kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa yanayohusiana na hali ya joto.


