24.3 C
New York

Fei Toto hatanii, atupia tena kubaki kileleni

Published:

NA Hassan Mwasha

NI kama kiungo wa Azam, Feisal Salum ‘Fei Toto’, amepania kuondoka na kiatu cha ufungaji bora msimu huu wa 2025-26 wa Ligi Kuu Bara.

Katika mchezo wao wa leo Juni 27, 2026, Azam wakiwa ugenini jijini Tanga, wamechomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji wao, Coastal Union.

Fei Toto akiwa sehemu ya kikosi, aliifungia Azam bao la pili dakika ya 43 baada ya Ahoutou Zouzou kutangulia dakika ya 40.

Kwa hesabu zilivyo, Fei Toto ameongeza moja na kufikisha mabao 16 msimu huu wa Ligi, hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa kiatu.

Katika nafasi ya pili, ni staa wa Yanga raia wa Uganda, Allan Okello ‘Star Boy’, ambaye amefikisha mabao 14 baada ya ‘hat-trick’ yake dhidi ya TRA United.

Ikumbukwe, nyota huyo wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, hajawahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara, licha ya misimu mingi aliyocheza akiwa na Singida, Yanga na sasa Azam.

Related articles

Recent articles