24.3 C
New York

32 Bora: Morocco kuendeleza ‘uteja’ kwa Uholanzi?

Published:

TORONTO, Canada

NI mtihani kwa timu zote mbili katika kuwania tiketi ya kwenda hatua inayofuata ya 16 Bora ya msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.

Timu hizo zitakutana Juni 30, 2026, kwenye Uwanja wa Monterrey, Mexico, ukiwa ni mtanange wa hatua ya 32 Bora ya michuano hiyo.

Morocco iliyoandika historia ya kuwa timu ya kwanza Afrika kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia, ilipofanya hivyo mwaka 2022, safari hii imevuka makundi ikiwa haijafungwa.

Ikiwa Kundi C, ilianza kwa sare dhidi ya Brazil, kisha ushindi mbele ya Scotland, kabla ya kuitandika Haiti mabao 4-2 katika mchezo wa mwisho.

Uholanzi, kwa upande wao, nao wameingia hatua ya 32 Bora baada ya kumaliza kileleni mwa Kundi F, ikizifunga Sweden, Tunisia, kisha sare mbele ya Japan.

Kwa rekodi, Uholanzi imeshinda mechi zote tatu ilizowahi kukutana na wawakilishi hao wa Afrika ya Kaskazini. Je, Morocco itakataa ‘uteja’ safari hii?

Vikosi: Uholanzi (4-3-3) – Verbruggen, Dumfries, Van Hecke, Van Dijk, Ake, Gravenberch, De Jong, Reijnders, Malen, Brobbey na Gakpo.

Morocco: (4-2-3-1) – Bono, Hakimi, Diop, Riad, Mazroaoui, El Aynaoui, Bouaddi, Diaz, Saibari, El Khannouss, na El Khaabi.

Related articles

Recent articles