24.3 C
New York

32 Bora: Paraguay siyo kinyonge kwa Ujerumani

Published:

MEXICO CITY, Ujerumani

ZITAKUTANA katika mchezo wa hatua ya 32 Bora msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia. Mechi itachezwa keshokutwa (Juni 29, 2026).

Licha ya kufungwa na Ecuador katika mchezo wa mwisho, Ujerumani imevuka makundi baada ya ushindi dhidi ya Curacao (7-1) na Ivory Coast (2-1).

Paraguay, kwa upande wao, ni wanufaika wa tiketi ya ‘tatu bora’ kwani walimaliza chini ya nafasi mbili za juu kwenye Kundi D.

Katika mechi yao ya kwanza, walitandikwa mabao 4-1 na Marekani, kisha wakashinda bao 1-0 dhidi ya Uturuki, kabla ya suluhu (0-0) waliyoipata mbele ya Australia.

Hata hivyo, licha ya Ujerumani kuonekana kuwa na nafasi kubwa ya ushindi, mechi dhidi ya Paraguay haijawahi kuwa rahisi kwa vigogo hao wa soka la Ulaya.

Katika mechi mbili walizokutana na Paraguay hivi karibuni, Ujerumani imeshinda moja (1-0) na kutoa sare moja (3-3).

Mechi ya kwanza ilichezwa Desemba 5, 2003 na ilikuwa ya Kombe la Dunia hatua ya 16 Bora na ya pili ilikuwa ya kirafiki katika kalenda ya FIFA.

Kwa takwimu hizo, ni wazi mchezo wa wiki ijayo si tu hautabiriki kwa Ujerumani, bali pia ni mgumu kwa Paraguay; yeyote anaweza ‘kupasuka’.

Mshindi wa mchezo huo huenda akakutana ana kwa ana na mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2018, Ufaransa.

Related articles

Recent articles