Na mwandishi wetu, Gazetini
ALIYEWAHI kuwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amekunwa na kiwango kizuri cha timu ya soka ya vijana wa U-17 ya Tanzania (Serengeti Boys) katika fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazoendelea nchini Morocco.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo, Serengeti Boys imeingia fainali baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Misri katika nusu fainali ya Mei 28, 2026 jijini Rabat.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Wenger, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Soka ya Shirikisho la mchezo huo duniani (FIFA), amesema Serengeti Boys haikubahatisha, bali imeonesha kiwango cha kuvutia.
Serengeti Boys iliingia hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa penalti dhidi ya vigogo wengine wa soka la Afrika, Algeria.
Licha ya kuingia fainali, tayari vijana hao wa Tanzania wameshajihakikishia tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu zitakazofanyika huko Qatar.


