19.8 C
New York

Rais Ruto awasili Tanzania kwa ziara ya siku mbili

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Rais wa Kenya, Dk. William Ruto amewasili nchini leo kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili, ambapo kesho Mei 5, 2026 atalihutubia Bunge la Tanzania, jijini Dodoma.

Ruto amepokelewa kwa gwaride la heshima na mwenyeji wake, Rais. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es Salaam ambapo pia watafanya mazungumzo yanayolenga  kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya.

Pia marais hao kwa pamoja wanatarajiwa kushiriki katika Jukwaa la Biashara litakalowakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi hizo mbili, kwa lengo la kuimarisha biashara na uwekezaji wa kikanda.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img