RABAT, Morocco
RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa [FIFA], Gianni Infantino, ameipongeza timu ya soka ya Wanawake ya U-17 ya Nigeria ‘Flamingos’ kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia.
Vijana hao wa Nigeria wametawazwa kuwa mabingwa baada ya kuwafunga wenzao wa Japan kwa kichapo cha mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa usiku wa jana Novemba 7, 2026.
Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa katika Uwanja wa Mohammed VI mjini Rabat, Morocco, Nigeria ilipata mabao yake kupitia kwa Awawu Bashiru na Oluebube Umejiaku, huku Fuki Ito akiifungia Japan bao la kufutia machozi.
Kwa ushindi huo, Nigeria inakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutwaa Kombe la Dunia la U-17 ya Wanawake.
“Pongezi kwa Nigeria, mabingwa wa Kombe la Dunia la U-17 kwa Wanawake hapa Rabat. Timu ya kwanza ya Afrika kufanya hivyo, pongezi nyingi kwa Nigeria. Walistahili kufika fainali,” amesema.
Katika hatua nyingine, Infantino alizipongeza Japan na Korea kwa kushika nafasi ya pili na ya tatu, pia Morocco kwa kuandaa fainali zilizofana.


