10.5 C
New York

Taifa Stars yapishana na makali ya Osimhen

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini – DAR

HII ni habari njema kwa mashabiki wa Taifa Stars, kwamba straika tishio wa timu ya soka ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Victor Osimhen, amefanyiwa upasuaji wa goti na huenda akawa nje kwa wiki tatu.

Stars itaifuata Nigeria katika mchezo wa kufuzu fainali za AFCON 2027, mchezo huo ukitarajiwa kuchezwa Novemba 13, 2026, kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabio nchini humo.

Sasa, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu yake ya Galatasaray, Osimhen atakosekana kwa kipindi kisichopungua wiki tatu baada ya upasuaji wa goti aliloumia katika mechi yao dhidi ya VfB Stuttgart.

Mshambuliaji huyo aliumia goti la kushoto na mabosi wa Galatasaray wamesema amefanyiwa upasuaji na daktari wa timu hiyo, Yener Ince.

Vyanzo mbalimbali vya habari nchini Uturuki vimeeleza kuwa Osimhen atarejea dimbani Novemba 24, 2026, siku watakayokuwa uwanjani kumenyana na Aston Villa.

Kwa ratiba hiyo, ni wazi pia Osimhen ataikosa mechi ya marudiano dhidi ya Stars, ambayo inatarajiwa kuchezwa Novemba 17, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex huko Visiwani Zanzibar.

Related articles

Recent articles