10.5 C
New York

Changamoto ya afya ya akili kwa wajawazito

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

CHANGAMOTO ya afya ya akili ni moja ya maeneo nyeti kwa sasa, ikipewa umuhimu mkubwa kutokana na athari zake si tu kwa mtu binafsi, bali pia kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Katika mataifa mengi, changamoto ya afya ya akili inapewa uzito mkubwa, ikitajwa kupunguza nguvu kazi, hivyo kuathiri kasi ya maendeleo.

Sasa, utafiti mpya wa Ofisi ya Sayansi na Teknolojia ya Uingereza (POST) umebaini kuwa wanawake wajawazito au waliotoka kujifungua huweza kuangukia kwenye changamoto ya afya ya akili.

Aidha, utafiti huo umeeleza zaidi, kwamba wengi kati ya wanawake waliojifungua na kupata changamoto hiyo huamua kujiua.

Utafiti huo ukitumia takwimu za mwaka 2021 hadi 2023, ulibaini kuwa mwanamke mmoja kati ya watatu waliopitia changamoto ya afya ya akili baada ya wiki sita au mwaka mmoja tangu ajifungue, alifariki kwa kujiua. Kwa upande mwingine, gharama za matibabu ya afya ya akili zimetajwa kuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa mgonjwa, hivyo kufikia uamuzi wa kujitoa uhai.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img