9.5 C
New York

Amorim kurudi EPL kuinoa Palace

Published:

LONDON, Uingereza

HUENDA kocha wa zamani wa Manchester United, Ruben Amorim, akawa na timu nyingine msimu ujao wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Mreno huyo alifungashiwa virago Januari, 2026 baada ya miezi 14 ya kuliongoza benchi la ufundi la Man United.

Amorim, ambaye amekuwa kimya tangu alipofungashiwa virago Old Trafford, kwa sasa anahusishwa na kibarua cha Oliver Glasner.

Glasner raia wa Australia, alishatangaza tangu Januari, 2026 kwamba huu ni msimu wake wa mwisho katika benchi la ufundi la Crystal Palace.

Kocha huyo ameripotiwa kuingia kwenye uhusiano mbaya na mabosi wa Palace, hiyo ikitajwa kuwa ndiyo sababu ya kuamua kuondoka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img