2.8 C
New York

Papa aingilia kati hali ya usalama Nigeria

Published:

LAGOS, Nigeria

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV, ametuma ujumbe wake wa kutaka kuimarishwa kwa hali ya amani nchini Nigeria.

Papa Leo ameyasema hayo katika hotuba yake ya Ibada ya Jumapili ya jana Februari 8, 2026.

Ujumbe wake huo umekuja baada ya watu wenye silaha kuua wanakijiji watatu na kuteka wengine 11, achilia mbali 170 waliuawa mwanzoni mwa wiki hii mjini Woro.

Januari, 2026, waumini wa Kikiristo zaidi ya 150 walitekwa katika matukio matatu tofauti ya watu wenye silaha kuvamia makanisa mjini Kaduna.

Katika hotuba yake, Papa amesema: “Ni huzuni kuona mashambulizi ya hivi karibuni katika jamii za Nigeria, ambayo yamesababisha watu kupoteza maisha.

“… Naamini kwamba mamlaka zitaendelea na jitihada za kuhakikisha hali ya usalama inarejea na raia wote wanakuwa kwenye amani.

“Hiayoria inatufundisha kuwa mikakati ya kiuchumi na nguvu za kijeshi hazina nafasi katika ubinadamu. Mustakabali mzuri hupatikana kwa watu kuheshimiana na kuishi kama ndugu.”

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img